Jinsi ya Kujisajili Premier Bet: Muongozo Hatua kwa Hatua

Last updated July 10, 2024

Wachezaji wapya wa michezo ya kubahatisha, yaani wanaobeti, hivi sasa wanaweza kujisajili Premier Bet Tanzania na kufungua akaunti zao za kubeti. Hali kadhalika, kujisajili na Premier Bet mtandaoni ni rahisi sana. Unaweza kujifunza zaidi jinsi ya kujisajili premier bet kupitia maelezo haya. 

Jinsi ya Kujisajili Premier Bet Tanzania

Wachezaji wote wanaotaka kuweka dau au kutumia namba (yaani code) ya Premier Bet, wanahitaji kwanza kufungua akaunti. Aidha, kujisajili Premier Bet kunahitaji kufuata hatua maalumu ambazo wachezaji wote wanatakiwa kuzipitia. Hapa chini, unaweza kupata maelezo ya hatua muhimu za jinsi ya kujisajili Premier Bet mtandaoni:   

Jinsi ya kufungua akaunti ya Premier Bet.

  1. Mosi, wachezaji wanatakiwa kutembelea tovuti rasmi ya Premier Bet.

  2. Ukishaingia kwenye tovuti ya Premier Bet, utabofya kitufe kilichoandikwa “Jisajili” kilichopo upande wa juu kulia mwa ukurasa mkuu wa tovuti.

  3. Wachezaji wanaotaka kujisajili Premier Bet Tanzania wanaweza kuchagua kati ya fomu ya usajili kwa haraka au fomu ya usajili kamilifu.

  4. Baada ya kubofya kitufe cha “Jisajili”, fomu ya kwanza kufunguka itakuwa ya usajili wa haraka.|

    Kuhusu fomu ya usajili wa haraka, wachezaji watajaza namba za simu na neno la siri watakalotumia kwenye tovuti hii. Vile vile wanatakiwa kuweka tiki kwenye visanduku ili kuthibitisha wana umri unaokubalika kisheria, na kwamba wanakubali vigezo na masharti.

  5. Mwishowe, ili kukamilisha ujazaji wa fomu ya haraka, wachezaji wanatakiwa kubofya kitufe cha “Tuma Code ya Usajili.”

  6. Aidha, wachezaji wanaweza kubofya kitufe cha “Tumia Fomu ya Usajili Kamilifu” ili kujisajili na kukamilisha akaunti zao za kubeti.

  7. Aidha, wachezaji wanatakiwa kujaza jina la kwanza, la ukoo, anwani ya barua pepe, namba ya simu, na neno la siri. Baada ya hapo, wanatakiwa bofya “Jisajili”

  8. Wachezaji wanaotaka kujisajili Premier Bet Tanzania, wanatakiwa kuthibitisha taarifa walizojaza ili kuziwezesha akaunti zao.

jinsi ya kujisajili premier bet

Jinsi ya Kujisajili Premier Bet Kwa Simu

Zaidi ya hayo, wanaobeti wanaweza kukamilisha mchakato wa usajili kwa kutumia simu zao. Watumiaji wa Android na iOS wanaweza kuifikia tovuti ya Premier Bet Tanzania kupitia vivinjari vya simu zao. Kisha, wanaweza kubofya kitufe cha “Jisajili” kilichopo sehemu ya juu ya kioo cha simu. Kwa nyongeza, wanatakiwa kukamilisha mchakato wa usajil kwa kujaza fomu ya usajili. 

Jinsi ya Kuweka Pesa na Premier Bet Tanzania

Kwa kawaida, wachezaji wapya wanaofungua akaunti kupitia Premier Bet Tanzania, hupendelea zaidi kutumia njia za malipo zilizopo. Ili kuweka pesa kwenye akaunti yako, itakubidi kwanza uingie kwenye tovuti kwa kutumia taarifa ulizotumia kujisajili. Ukishaingia, bofya kitufe kilichaondikwa  “Weka Pesa”. Aidha, unatakiwa kuongeza kiasi cha pesa unachotarajia kuweka. Baada ya hapo, unatakiwa kuchagua njia ya malipo unayopenda kuitumia.

Kwa sasa, Premier Bet inakupa njia mbalimbali za kuweka pesa kwenye akaunti yako. Njia hizo ni pamoja na Airtel Money, Tigo Pesa, Vocha, na M-Pesa.

Jinsi ya Kutoa Pesa Premier Bet Tanzania

Endapo unataka kutoa pesa, inabidi kwanza uingie kwenye akaunti yako ya kubeti. Ukishaingia, utabofya kitufe cha “Toa Pesa” ili uweze kuingiza kiwango cha pesa unachotaka kutoa.

Hali kadhalika, wachezaji wanaweza kuchagua mojawapo kati ya njia mbalimbali zilizopo za malipo. Njia hizi utaziona baada ya kubofya menyu kunjuzi, yaani menyu yenye kimshale kinachotazama chini. Wateja wa Premier Bet wanaweza kutoa pesa kwa kutumia njia zile zile zinazotumika kuweka pesa. Njia hizi ni pamoja na M-Pesa, Vocha, Airtel Money, na Tigo Pesa.

Jinsi ya Kuweka Mkeka na Premier Bet Tanzania 

Wateja wengi wapya wa Premier Bet watapenda kufahamu jinsi ya kuweka mkeka na Premier Bet Tanzania. Baada ya kuweka pesa kwenye akaunti, wanaobeti wanaweza kuchagua tukio, yaani event moja, au kuchagua event zaidi ya moja wanazotaka kuzijumuisha kwenye mikeka yao.

Mbali na hayo, wachezaji wanaweza kutumia fursa kupitia michezo mbalimbali kama vile soka, mpira wa meza (yaani tennis), mpira wa kikapu, na besiboli. Pia wanaweza kuchagua matukio kutoka kwenye ligi mbalimbali kama vile Bundesliga, MLB, Mashindano ya Tenisi ya French Open, au NBA.

Baada ya kuchagua tukio au event wanazotaka kuweka mkeka, wanaobeti wanatakiwa kubofya kwenye odd wanayodhani watashinda. Baada ya hapo, watatakiwa kuweka kiwango cha pesa wanachotarajia kuwekeza kwenye mkeka husika, kisha bofya “Weka Mkeka”

Kwa njia ile ile, wanaobeti wanaweza kwenda kwenye “Mkeka Mubashara”, yaani Live Betting na kuweka mkeka huku tukio likiendelea. Wanaobeti wanaweza kutumia Mkeka Mubashara kupitia matukio yanayoendelea kwenye michezo mbalimbali. Aidha, ni muhimu kutaja kwamba, wachezaji wanaweza kuweka mkeka kabla ya mchezo na pia wakati mchezo unaendelea. Wanaweza kufanya hivyo kupitia kompyuta zao za mezani na vifaa vya mkononi kama vile simu na kompyuta mpakato.

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara Kuhusu Jinsi ya Kujisajili Premier Bet Tanzania 

Kwa kusoma maswali haya yaulizwayo mara kwa mara, unaweza kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kujisajili Premier Bet Tanzania.

Je, Premier Bet ni halali Tanzania?

Ndiyo, Premier Bet Tanzania inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na imepewa leseni na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania. Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ni taasisi ya serikali. Wenye umri unaokubalika kisheria ambao wanaishi Tanzania, wanaweza kujisajili Premier Bet Tanzania na kufungua akaunti.

Ni nani wanaweza kufungua akaunti na Premier Bet Tanzania?

Ili kujisajili Premier Bet Tanzania, mchezaji anatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea. Zaidi ya hilo, wanaotaka kujisajili Premier Bet Tanzania wanatakiwa kuwa wakazi wa Tanzania.

Unawezaje Kuthibitishwa na Premier Bet?

Ukitaka kuithibitisha akaunti yako, kwenye fomu ya usajili utajaza jina lako la kwanza na la ukoo kama yanavyoonekana kwenye kitambulisho. Aidha, unatakiwa kujaza namba yako ya simu pamoja na anwani yako ya barua pepe unayoitumia mara kwa mara.

Vipi Kuhusu Jinsi ya Kucheza Premier Bet mtandaoni?

Wanachama wote waliojisajili wanaweza kuweka mikeka yao mtandaoni kwa kutumia kompyuta au simu za mkononi. Ili kuweza kuweka dau kupitia tovuti hii, unatakiwa kwanza kuingia kwenye akaunti yako kwa kutumia taarifa ulizotumia kujisajili. Baada ya kuongeza pesa kwenye salio lako, hatimae unaweza kucheza kwa kuchagua odd unazodhani zitashinda.

Unafanyaje malipo Premier Bet kwa kutumia Airtel Money?

Kuweka pesa kwa kutumia Airtel Money, unatakiwa kuingia kwenye akaunti yako, kisha kwenye ukurasa wa kuweka pesa. Baada ya hapo, utachagua Airtel Money na kuongeza kiwango chapesa unachotaka kuweka. Aidha, itakubidi kujaza namba yako ya simu sehemu iliyoandikwa “Namba Mpya ya Simu” kisha bofya kitufe cha “Tuma”.

18+ | Please play responsibly | Terms and Conditions apply | Commercial Content